Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kugundua mapema changamoto za kiafya zinazoweza kuathiri masomo na maisha ya kila siku ya wanafunzi, pamoja na kuhamasisha tabia za afya njema.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Tarehe 20/08/2025 – Dar -es- Salaam, limefanyika zoezi laUpimaji wa Afya kwa Wanafunzi wa Kiume wa Chuo cha Al-Mustafa(s), kilicho Mbezi Beach.
Katika kuendeleza juhudi za kuhakikisha ustawi wa wanafunzi, Chuo cha Al-Mustafa(s) kilicho katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam - Tanzania, kiliandaa siku maalumu ya kufanya vipimo vya afya kwa wanafunzi wa kiume.
Katika zoezi hili, Daktari na mhudumu wa afya kutoka nchini Iran, alihudumia Wanafunzi kwa kuwapima vipimo vya msingi kama vile:
1_Shinikizo la damu.
2_Kiwango cha sukari mwilini.
3_Uzito na urefu kwa ajili ya kufuatilia hali ya lishe.
4_Vipimo vya macho na masikio.
5_Mashauriano ya kiafya na ushauri wa lishe.
Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kugundua mapema changamoto za kiafya zinazoweza kuathiri masomo na maisha ya kila siku ya wanafunzi, pamoja na kuhamasisha tabia za afya njema.
Viongozi wa chuo walimshukuru daktari huyu kwa kujitolea na kusisitiza kuwa vipimo vya afya vitakuwa sehemu ya mpango endelevu wa huduma kwa wanafunzi wote, wakiwemo wa kike katika awamu zijazo.
Wanafunzi nao walionyesha furaha na kufarijika kwa huduma waliyoipata, huku wakipata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu afya na namna ya kujikinga na magonjwa ya kisasa kama vile shinikizo la damu, kisukari na msongo wa mawazo.
Your Comment